Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Twiga Stars, Bakari Shime amesema wamefanya makosa na kukubali kichapo nyumbani cha mabao 3-0 dhidi ya Afrika Kusini lakini anaamini watapindua meza katika mchezo wa marudiano na ugenini.
Twiga jana Ijumaa ilipoteza mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na sasa wanahitaji ushindi nchini Afrika Kusini kujihakikishia ushiriki wa Olimpiki kwa Wanawake.
Shime alisema wamecheza na timu kubwa na wamepoteza kutokana na makosa yaliyojitokeza uwanjani, wakipoteza nafasi nyingi pia za kufunga mabao lakini wanarekebisha makosa yao tayari kwa mcheozo wa marudiano.
“Sasa tumejipanga vizuri kwenda kufanya vizuri katika mchezo wetu wa marudiano, tunatambua ukubwa wa Afrika Kusini na tunaenda kupambana kutafuta matokeo chanya,” alisema Shime.
Naye Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema kikosi cha Twiga Stars kimesafiri leo Jumamosi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.
Kimataifa Twiga Stars kupindua meza
Twiga Stars kupindua meza
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
