Sydney, Australia
Morocco imepata ushindi wa kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia za Wanawake ikiilaza Korea Kusini bao 1-0 huku gumzo akiwa beki wa timu hiyo, Nouhaila Benzina (pichani) kuwa mchezaji wa kwanza kuvaa hijab kwenye michuano hiyo.
Bao pekee la Morocco katika mechi hiyo ya Kundi H iliyopigwa leo Jumapili lilifungwa kwa kichwa na Ibtissam Jraidi katika dakika ya sita, bao lililotokana na krosi iliyochongwa na Hanane Ait Elhaj.
Matokeo hayo ya kwanza kwa Morocco yanaipa heshima timu hiyo iliyo nafasi ya 72 kwa viwango vya Fifa dhidi ya wapinzani wao ambao wapo nafasi ya 17 na walipewa nafasi kubwa ya kutoka na ushindi.
Akizungumzia ushindi huo, Jraidi alisema, “Tunashukuuru juhudi zetu zimelipa, ushindi huu ni wa Morocco na Waarabu, ni matunda ya kazi ngumu.”
Mambo yalikuwa magumu kwa Morocco katika mechi yake ya kwanza ilipolala kwa mabao 6-0 mbele ya Ujerumani kabla ya kupokea kichapo kingine cha mabao 2-0 mbele ya Colombia lakini ilionekana kuwa timu tofauti mbele ya Korea Kusini.
Ukiachana na matokeo hayo, gumzo lilikuwa ni beki wa Morocco, Benzina ambaye amecheza mechi yake ya kwanza kwenye fainali hizo na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuvaa hijab katika fainali za Kombe la Dunia za Wanawake.
Benzina alikuwa mchezaji wa akiba katika mechi dhidi ya Ujerumani lakini hakupata nafasi na anacheza soka nchini Morocco akiwa vazi hilo la kuhifadhi kichwa au hijab kama ilivyozoeleka mbele ya wengi.
Fifa kwa mara ya kwanza iliruhusu wanasoka wanawake kuvaa vazi hilo kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
Matokeo fainali za Kombe la Dunia Wanawake
Korea Kusini 0-1 Morocco
Norway 6-0 Philippines
Switzerland 0-0 New Zealand
Ujerumani 1-2 Colombia
Ufaransa 2-1 Brazil
Panama 0-1 Jamaica
Sweden 5-0 Italia
Kombe la Dunia Nouhaila, hijab ya kwanza Kombe la Dunia
Nouhaila, hijab ya kwanza Kombe la Dunia
Related posts
Read also