Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo ametuma ndege maalum iliyobeba vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea katika nchi za Uturuki na Syria na kuua watu zaidi ya 50,000.
Tetemeko hilo lililotokea Februari 8 pia lilisababisha watu zaidi ya 500,000 kuhamishwa katika makazi yao huku habari zaidi zikidai kuwa nyumba zaidi ya 160,000 ziliharibiwa na nyingine kubomoka kabisa.
Ronaldo ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, amewanunulia wahanga hao, madawa, nguo, mahema, magodoro, vyakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto.
Mwanasoka huyo nyota wa zamani wa Man United na Real Madrid, pia alisaidia kuitimiza ndoto ya mtoto wa Syria aliyewaambia waokoaji kwamba anataka kukutana na nyota huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 38.
Mtoto huyo wa kiume, Nabil Saeed pia ombi hilo lilifanikishwa kupitia mitandao ya kijamii na alialikwa kushuhudia mechi ya Al Nassr dhidi ya Al Batin, mechi ambayo Al Nassr ilishinda kwa mabao 3-1 na mtoto huyo kupata nafasi ya kupiga picha na Ronaldo.
“Nilipomuona Ronaldo niliona kama ilikuwa ndoto, sikuamini kama ndoto hii ingefikia mwisho, niliomba Mungu isiishie kuwa ndoto, natamani kila mtu aonane na Ronaldo, ni mtu mzuri,” alisema Nabil.
Kimataifa Ronaldo asaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Uturuki
Ronaldo asaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Uturuki
Read also