Na mwandishi wetu
Bao pekee la penalti iliyopigwa na Benard Morisson limeiwezesha Yanga kutoka na pointi tatu muhimu leo dhidi ya Geita Gold katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC ingawa mazingira ya penalti hiyo yameendelea kuwa mjadala kwenye mitandao ya kijamii nchini.
Yanga iliyokuwa ugenini CCM Kirumba mbele ya Geita Gold ilipata penalti hiyo muda mfupi kabla ya kumalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza baada ya mchezaji wa Geita kuunawa mpira ingawa Geita walipinga penalti hiyo kwa madai kwamba mchezaji haukuunawa mpira huo ndani ya eneo la penalti.
Hata hivyo wakati mijadala ikiendelea, matokeo ya leo yanaifanya Yanga kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi katika ligi hiyo hadi kufikia mechi 45 lakini pia timu hiyo sasa inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 20 ikifuatiwa na Mtibwa yenye pointi 15 ambayo kesho itaumana na Simba inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14.
Soka Bao la penalti laibeba Yanga
Bao la penalti laibeba Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
