Amsterdam, Uholanzi
Mastaa Kylian Mbappe wa Ufaransa na Cristiano Ronaldo wa Ureno wamezifungia timu zao mabao na kuziwezesha kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 24 zitakazofanyika mwakani nchini Ujerumani.
Timu nyingine iliyopata ushindi katika mechi hizo zilizochezwa jana Ijumaa na kufuzu ni Ubelgiji na kuzifanya timu hizo tatu ‘kutangulia’ nchini Ujerumani.
Mabao mawili ya Mbappe yaliiwezesha Ufaransa kutoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Uholanzi na huo kuwa ushindi wa sita kwa Ufaransa iliyo katika Kundi B.
Mbappe aliandika bao la kwanza dakika ya saba akiunganisha krosi ya Jonathan Clauss na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Uholanzi, Bert Verbruggen kabla ya kufunga bao la pili dakika ya 53 akiitumia pasi ya Adrien Rabiot.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu katika mechi za karibuni na timu yake ya PSG, mabao yake yalimfariji kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps ambaye alisema hana cha kuhofia kwa mchezaji huyo ambaye amedhihirisha uwezo na ubora wake.
Bao pekee la Uholanzi lilipatikana dakika ya 10 kabla ya mpira kumalizika mfungaji akiwa ni kiungo wa Feyenoord, Quilindschy Hartman.
Mabao mawili ya Ronaldo yaliiwezesha Ureno kutoka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Slovakia na kufuzu moja kwa moja huku Ronaldo akiimarisha rekodi yake ya mabao na timu hiyo kufikia 125 katika mechi 202.
Bao jingine la Ureno lilifungwa na Goncalo Ramos kwa kichwa wakati yale ya Slovakia yalifungwa na David Hancko na Stanislav Lobotka.
Nao Ubelgiji walipata ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Austria mjini Vienna wakineemeka na mabao ya
Romelu Lukaku, Dodi Lukébakio aliyefunga mawili wakati mabao ya Austria yalifungwa na Konrad Laimer na Marcel Sabitzer.
Matokeo ya mechi za kufuzu Euro 24…
Iceland 1-1 Luxembourg
Liechtenstein 0-2 Bosnia-Herzegovina
Ureno 3-2 Slovakia
Uholanzi 1-2 UfaransaT
Jam Ireland 0-2 Ugiriki
Estonia 0-2 Azerbaijan
Austria 2-3 Ubelgiji
Mechi za kufuzu Euro 2024 zinazochezwa leo Jumamosi
Kask Ireland v San Marino
Ukraine v Kask Macedonia
Italia v Malta
Bulgaria v Lithuania
Hungary v Serbia
Slovenia v Finland
Denmark v Kazakhstan
Kimataifa Ufaransa, Ureno zafuzu Euro 2024
Ufaransa, Ureno zafuzu Euro 2024
Read also