Na mwandishi wetu
Timu ya Simba imeendelea kuwa gumzo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoa wachezaji wanne kwenye kikosi bora cha wiki cha mzunguko wa tano wa michuano hiyo.
Simba imetoa idadi ya wachezaji hao waliotangazwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kutokana na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni beki Shomari Kapombe, kiungo Clatous Chama aliyefunga mabao matatu, Sadio Kanoute aliyefunga mawili na mshambuliaji Jean Baleke aliyefunga mawili pia katika mtanange huo.
Wachezaji wengine wanaounda kikosi hicho ni Mahmoud Kahraba, Percy Tau kutoka Al Ahly, Zakaria Draoui, Mouad Haddad (RC Belouizdad), Arsène Zola (Wydad Casablanca), Patou Simbi (AS Vita) na kipa Ronwen Williams wa Mamelodi Sundowns.
Pia, Chama na Kanoute wamechaguliwa kuwania nafasi ya mchezaji bora wa wiki wa michuano hiyo kutokana na viwango walivyoonesha, wakichuana vikali na wachezaji wa Al Ahly, Tau na Karhaba.
Ahly ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Cotton ambapo Karhaba alifunga mabao matatu na Tau alitupia bao moja.
Leo jioni anatarajiwa kutajwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho ambacho baada ya kusitishwa kwa zoezi la upigwaji kura Kwa wachezaji hao kwenye ukurasa rasmi wa Twitter wa Caf wa michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.
Chama na Kanoute pia wameingia kwenye orodha ya mabao matano bora ya wiki. Bao la Chama liliolingia kwenye orodha hiyo ni lile alilofunga kwa adhabu ndogo dakika ya 10 na la Kanoute lile alilofunga kwa shuti kali dakika ya 87.
Kimataifa Simba gumzo CAF
Simba gumzo CAF
Read also