Na mwandishi wetu
Kikosi cha timu ya Yanga kesho Jumatano kinatarajiwa kurejea mzigoni na kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya katika kambi itakayofanyika Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi yao, Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema baada ya kukamilisha suala la upimaji afya kwa wachezaji wote juzi na jana, timu iko tayari kuanza maandalizi.
Alisema kikosi hicho chini ya kocha mpya, Miguel Gamondi kitaanza progam ya mazoezi kwa vipindi viwili asubuhi na jioni, akisisitiza kuwa wamechagua kufanya kambi nyumbani sababu wanaamini kuna vifaa vya kisasa, lakini pia kuwapa nafasi wachezaji wanaotoka mbali kutulia sehemu moja.
“Ni vizuri kufanya maandalizi sehemu tofauti lakini tunachoangalia ni kuwa na vifaa vya kuwaandaa wachezaji, muda wa kutekeleza hayo, wachezaji wametoka mapumzikoni, wachezaji wanatoka safari ndefu tukaona tutawachosha wachezaji bora tubaki nyumbani,” alisema.
Mpaka sasa Yanga ikiwa hatua za mwisho kuanza kambi, imemtangaza mchezaji mmoja pekee waliyemesajili kuelekea msimu ujao ambaye ni mzawa Nickson Kibabage aliyetokea Singida Fountain Gate.
Wengine wanaotajwa kuwa tayari wamemalizana nao ingawa haijawawekwa hadharani ni Gift Fred kutoka SC Villa ya Uganda, Max Nzegeli kutoka Maniema ya DR Congo.
Soka Gamondi kuanza kazi Jtano
Gamondi kuanza kazi Jtano
Read also