London, England
Kiungo wa Newcastle, Sandro Tonali amekutwa na hatia ya kwenda kinyume na kanuni za soka baada ya kubainika kujihusisha na mchezo wa kamari katika mechi za soka na sasa anatakiwa kujieleza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha Soka England (FA), Tonali anadaiwa kuvunja moja ya kanuni za FA kwa kucheza kamari katika mechi za soka kati ya Agosti 2023 na Oktoba 2023 na anatakiwa hadi Aprili 5 awe amejibu madai hayo.
Tonali (pichani juu) aliyejiunga na Newcastle Julai mwaka jana akitokea AC Milan, Oktoba mwaka jana FA ilimfungia miezi 10 baada ya kubainika kujihusisha na mchezo wa kamari katika mechi za soka nchini Italia.
Hatua ya FA kumfungia mchezaji huyo ilikuja baada ya uchunguzi uliofaywa na waendesha mashtaka wa mjini Turin na siku chache baadaye wakala wake alinukuliwa akisema kwamba mchezaji huyo ana ‘maradhi’ ya kupenda kujihusisha na kamari.
Taarifa ya klabu ya Newacastle iliyopatikana kwenye mitandao ya kijamii ilieleza kuwa Tonali alishiriki kutoa ushirikiano wakati wote wa uchunguzi na klabu yake ipo pamoja naye.
Tonali kwa msimu huu ameichezea Newcastle mechi 11 na kuifungia bao moja na anakuwa mchezaji wa pili kufungiwa kwa kujihusisha na uchezaji kamari baada ya Ivan Toney wa Brentford.
Toney alifungiwa miezi minane na kutozwa faini ya Pauni 50,000 baada ya kukiri kuvunja kanuni ya kwa kujihusisha na uchezaji kamari kinyume na taratibu.
Toney alimaliza adhabu yake Januari mwaka huu na mapema mwezi huu aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England na kuifungia bao Jumanne iliyopita katika mechi dhidi ya Ubelgiji iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Kimataifa Tonali ategwa sakata la kamari
Tonali ategwa sakata la kamari
Related posts
Read also