Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappe huenda akaikosa mechi yao ya Mei 10 dhidi ya Barcelona maarufu El Clasico kutokana na matatizo ya misuli ya mguu wa kushoto.
Kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa amesema kuwa Mbappe ambaye hadi sasa amefunga mabao 28 ya ligi msimu huu, alijisikia vibaya katika mechi dhidi ya Real Betis iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na akaomba afanyiwe mabadiliko.
Kuumia kwa Mbappe pia kumeibua hofu kwenye timu ya taifa ya Ufaransa inayojiandaa kumtumia mchezaji huyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazoanza mwezi ujao nchini Marekani, Canada na Mexico ambapo Ufaransa itacheza mechi ya kwanza Juni 16 dhidi ya Senegal.
Mbali na Mbappe ambaye suala lake limewekwa wazi, Real Madrid pia imepata pigo kwa beki wake Eder Milito kufanyiwa upasuaji nchini Finland baada ya kupata majeraha ya misuli katika mechi dhidi ya Alaves.
Militio, 28, ambaye anatokea Brazil alifanyiwa mabadiliko kabla ya mapumziko kwenye mechi hiyo dhidi ya Alaves ambayo Real Madrid walitoka na ushindi wa mabao 2-1.
Hii si mara ya kwanza kwa Milito kukutana na tatizo kama hilo, alijikuta katika hali hiyo msimu wa 2023-24 na msimu uliofuata wa 2024-25 wakati msimu huu wa 2026-27 amecheza mechi 16 tu za La Liga.
Kimataifa Mbappe kuikosa El Clasico
Mbappe kuikosa El Clasico
Read also
