Barcelona, Hispania
Wanasoka mastaa wa klabu ya PSG, Lionel Messi na Neymar wanaweza tu kurudi klabu yao ya zamani ya Barcelona bila ya ada ya uhamisho.
Rais wa Barcelona au Barca, Joan Laporta amesema kwamba itakuwa haina maana kulipa fedha kwa wachezaji hao ambao wote waliwahi kuichezea klabu hiyo.
“Nani asiyemtaka Ney (Neymar), ni mchezaji wa kipekee lakini ana miaka mitatu katika mkataba wake na PSG ni kama vile fedha imemdhibiti, namna pekee ya yeye kurudi Barca ni pale atakapokuwa huru, itakuwa ajabu kulipa ada ya uhamisho kwa mchezaji ambaye mliwahi kuwa naye,” alisema Laporta.
“Leo aliondoka alivyoondoka, sote tulipenda amalizie soka lake hapa lakini kwa sababu ya mfumo wa La Liga wa fair play na kwa sababu ya ofa ya PSG haikuwezekana kwake kumalizia soka hapa,” aliongeza.
Laporta pia alisisitiza kuwa kama mchezaji huyo anataka kurudi itakuwa ni pale atakapokuwa huru kusiwe na ada ya uhamisho na hapo hapo watu wa benchi la ufundi watakuwa na uamuzi kuhusu kama anafaa kuwa kwenye timu mpya au hafai.
Neymar mwenye umri wa miaka 30 sasa, alisaini mkataba mpya na PSG mwaka jana majira ya kiangazi lakini majaaliwa yake katika klabu hiyo yamekuwa katika uchunguzi hasa baada ya Kylian Mbappe kuamua kuongeza mkataba kwenye klabu hiyo.
Mchezaji huyo amekuwa akiichezea PSG tangu mwaka 2017 baada ya timu hiyo kulipa ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia ya Euro milioni 222 ili kumtoa Barca wakati Messi ambaye ana miaka 34 na alitua PSG mwaka jana majira ya kiangazi, amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na klabu hiyo.
Kimataifa Bosi atoa sharti Neymar, Messi kurudi Barca
Bosi atoa sharti Neymar, Messi kurudi Barca
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
