Dortmund, Ujerumani
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu, Borussia Dortmund imefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiichapa PSV Eindhoven mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Jadon Sancho na Marco Reus.
Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa jana Jumatano usiku yanawafanya Dortmund waliokuwa wenyeji wa mchezo huo kufuzu hatua hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza.
Sancho nyota aliyejiunga na Dortmund kwa mkopo Januari mwaka huu akitokea Man United baada ya kutibuana na kocha wake, Erik ten Hag, hata hivyo hakumaliza mechi hiyo baada ya kutolewa dakika ya 79 ikidaiwa kuwa alipata matatizo ya misuli.
Nafasi ya Sancho aliingia Reus ambaye naye aliingia na neema baada ya kuipatia Dortmund bao la pili katika dakika tano za nyongeza.
Kwa Sancho hakuishia kufurahia bao hilo tu badala yake alijivunia kubeba tuzo ya nyota wa mchezo aliyoipata kwa kuonesha kiwango kizuri katika mechi hiyo.
Wiki iliyopita, Sancho pia alifunga bao lake la kwanza tangu kujiunga na timu hiyo katika mechi ya Bundesliga wakati Dortmund ilipoichapa Werder Bremen mabao 2-1.
Droo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika Ijumaa hii ambapo timu zote zilizofuzu hatua hiyo zitawajua wapinzani wao.
Timu zilizofuzu robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Arsenal
Atletico Madrid
Barcelona
Bayern Munich
Borussia Dortmund
Man City
PSG
Real Madrid
Kimataifa Sancho aipeleka Dortmund robo fainali Ulaya
Sancho aipeleka Dortmund robo fainali Ulaya
Read also