Milan, Italia
Klabu ya Inter Milan ya Italia imemsajili kipa wa Cameroon, Andre Onana ambaye amewahi kufungiwa kujihusisha na soka kwa miezi 12 kwa kilichodaiwa kuwa ni kutumia madawa ya kuongeza nguvu.
Onana ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano na Inter akiwa mchezaji huru, alikuwa akiichezea klabu ya Ajax ya Uholanzi na alikutwa na majanga hayo Februari mwaka jana akiwa ameichezea mechi kadhaa Ajax ambayo hata hivyo iliibuka kinara wa ligi kuu nchini humo maarufu Eredivisie.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 sasa na ambaye aliiwahikisha vyema Cameroon kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) hadi kushika nafasi ya tatu, katika klabu ya Inter anatarajia kuwa mbadala wa kipa mkongwe Samir Handanovic mwenye umri wa miaka 37.
Katika miaka yake saba na nusu aliyoichezea Ajax, Onana ameweka rekodi ya kucheza mechi 214 za mashindano mbalimbali na sasa anaingia katika changamoto mpya kwenye Ligi Kuu Italia maarufu Serie A akiwa ni usajili mwingine baada ya kiungo Kristjan Asllani kutoka Empoli na mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka Chelsea ambaye hata hivyo aliwahi kuichezea Inter hapo kabla.
Onana anakuwa mchezaji wa nne wa Cameroon kukipiga Inter akitanguliwa na Samuel Eto’o, Pierre Wome na Daniel Boumsong, Novemba mwaka huu anatarajia kuiwakilisha Cameroon akiwa kipa namba moja kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar.
Kimataifa Kipa Onana atua Inter Milan
Kipa Onana atua Inter Milan
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
