Madrid, Hispania
Real Madrid ya Hispania imefikia katika hatua nzuri kumsajili kiungo wa timu ya Taifa ya England na klabu ya Borussia Dortmund, Jude Bellingham kwa ada inayotajwa kufikia Euro milioni 100.
Bellingham ambaye anatakiwa na klabu kadhaa kubwa za Ulaya ikiwamo Man City, alitua Dortmund Julai 2020 akitokea Birmingham na amekuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo kabla ya kung’ara na England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022.
Real Madrid hata hivyo inatakiwa ijipange hasa ili kumpata mchezaji huyo ambaye zipo habari kwamba thamani yake inatajwa kuzidi Euro milioni 100 ambazo vigogo hao wa Hispania wanajipanga kutoa.
Matumaini ya Real Madrid yamekuwa makubwa baada ya Bellingham mwenyewe kukataa ofa ya mkataba wa kuendelea kukipiga na Dortmund.
Bellingham ambaye ndio kwanza ana miaka 19, ameichezea Dortmund mara 40 msimu huu na kuifungia mabao 11 akionyesha kiwango cha hali ya juu.
Na ingawa Real Madrid imekuwa na matumaini makubwa, Man City nayo haijakata tamaa katika kuiwania saini ya mchezaji huyo ili aungane na kinara wao wa mabao, Erling Haaland ambaye pia amewahi kuichezea Dortmund kabla ya kutua Man City.
Kimataifa Bellingham asubiriwa Real Madrid
Bellingham asubiriwa Real Madrid
Read also