Na mwandishi wetu
Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC leo Jumapili baada ya kuichapa Singida Fountain Gate katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la Liti mjini Singida.
Ushindi huo sasa umeifanya Simba kufikisha pointi 15 katika mechi tano ikiwa haijapoteza hata mechi moja na imeizidi Yanga kwa pointi tatu.
Simba ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 26 ya mchezo huo, bao lililofungwa na Saido Ntibazonkiza akiitumia vizuri pasi ya Dennis Kibu na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Simba wakiwa mbele.
Dakika saba baada ya kuanza kipindi cha pili, Deus Kaseke aliwanyamazisha mashabiki wa Simba baada ya kuisawazishia timu yake bao.
Bao la Kaseke lilionekana kuamsha ari kwa timu hiyo na kuibua matumaini ya kuwadhibiti Simba lakini juhudi za timu hiyo zilikwama katika dakika ya 82 baada ya Moses Phiri kuandika bao la pili akiitumia pasi ya Luis Maquissone.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Tanzania Prisons ikiwa nyumbani imeichapa Mtibwa Sugar mabao 3-2.
Soka Simba yarejea kileleni ligi kuu
Simba yarejea kileleni ligi kuu
Read also