Roma, Italia
Kocha wa Roma, Jose Mourinho amemsajili katika timu hiyo aliyekuwa kiungo wa Man United, Nemanja Matic ikiwa ni mara yake ya tatu kumsajili mchezaji huyo.
Mourinho na Matic walikuwa pamoja Chelsea mwaka 2014 wakati Mourinho akiwa kocha katika klabu hiyo na miaka mitatu baadaye akiwa Man United alimsajili mchezaji huyo kabla ya kuondoka na kumuacha.
Matic mwenye umri wa miaka 33 sasa, mkataba wake na
Man United umefikia ukomo mapema mwezi huu na tayari anaelekea Roma kuungana na Mourinho ambaye hivi karibuni aliiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Europa Conference League.
Akizungumzia uamuzi wa Mourinho kumsajili, kiungo huyo kutoka Serbia alisema kwamba anaamini Mourinho ndiye kocha sahihi kwake. “Tuliwahi kufanya kazi pamoja, tuna muunganiko mzuri na yeye ndio sababu ya mimi kuja hapa.”
“Si jambo rahisi tu kufanya naye kazi, kunaweza kuwa na ugumu lakini ni kocha mshindi na hakika ni aina ya kocha hasa ninayemhitaji na ninachotaka katika maisha yangu ya soka ni kupata ushindi, anahamishia nguvu kwa wachezaji, naamini tunaweza kufanya mambo makubwa pamoja.”
Wakiwa Chelsea, Matic alikuwa mchezaji muhimu wa Mourinho mwenye uhakika wa namba na pia alikuwa na umuhimu wake Man United chini ya Mourinho akicheza mechi 35 za Ligi Kuu England katika mwaka wake wa kwanza, zote akicheza kuanzia kipindi cha kwanza kasoro mechi mbili tu.
Mourinho ameamua kumsajili Matic Roma ili kuiongezea nguvu safu ya kiungo ya timu hiyo wakati huu ikijiandaa kuagana na Henrikh Mkhitaryan, nyota mwingine wa zamani wa Man United.
Kimataifa Matic amfuata Mourinho Roma
Matic amfuata Mourinho Roma
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
