Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata amesema kipigo walichokipata cha mabao 2-0 dhidi ya Ihefu jana, kimeonesha namna gani timu hiyo inahitaji kufanya usajili kuanzia mabeki, viungo mpaka washambuliaji.
Makata amezungumza hayo ikiwa ni mechi ya pili kuiongoza Ruvu tangu akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kutoka kwa Charles Mkwasa aliyejiuzulu. Mechi ya kwanza ilikuwa ya Kombe la FA ambayo timu hiyo ilicheza na Ndanda na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
“Kulingana na hali ilivyo kunahitajika marekebisho mengi ndani ya timu kwa sababu kuna wachezaji kama nane wa kikosi cha kwanza wameenda kozi, tunahitaji kurekebisha kwenye usajili huu kuanzia ulinzi, viungo mpaka washambuliaji na kutengeneza mfumo wa kuleta ushindani zaidi.
“Mfano kwenye mechi hii viungo walianza vizuri lakini muda ulivyozidi kwenda walipoteza umakini na hata mabeki tangu kwenye mechi ambazo sijafika hapa mabao mengi ya kufungwa yalitokana na makosa yetu, kwa hiyo juhudi zitafanyika kupata wachezaji wenye ubora wa kutengeneza kikosi,” alisema Makata.
Naye kocha msaidizi wa Ihefu, Zuberi Katwila alisema: “Tunashukuru kumaliza mechi salama na kupata pointi tatu, tumepata nafasi nyingi lakini tumefanikiwa kutumia mbili ingawa tangu mwanzo mchezo ulionekana wa kwetu lakini bado tunaendelea kutengeneza kikosi kupitia dirisha dogo la usajili.”
Soka Makata: Ruvu inahitaji kusajili wapya
Makata: Ruvu inahitaji kusajili wapya
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
