Na mwandishi wetu
Vigogo vya soka nchini, Simba na Yanga hatimaye wamewajua wapinzani wao kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho ambapo Simba itaanza kuumana na Horoya ya Guinea wakati Yanga ikiumana na Monastir ya Tunisia.
Michuano hiyo ambayo inaandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Makundi ya timu hizo yamepangwa Jumatatu hii na ambapo Simba itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa imepangwa Kundi C ambalo lina timu za Raja Casablanca, Horoya ya Guinea na Vipers ya Uganda wakati Yanga imepangwa Kundi D lenye timu ya TP Mazembe ya DR Congo, Monastir na Real Bamako ya nchini Mali.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa, mechi za kwanza zitachezwa kati ya Februari 10 na 11, 2023 ambapo Simba itakuwa ugenini na mechi za pili zitachezwa Februari 17 na 18 ambapo Simba itakuwa nyumbani ikiumana na Raja Casablanca. Katika mechi yake ya tatu Simba itakuwa nyumbani dhidi ya Vipers.
Kwa upande wa Kombe la Shirikisho mechi za kwanza zitachezwa kuanzia Februari 10 ambapo Yanga itakuwa ugenini na itacheza mechi yake ya pili Februari 19 ikiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe na kumalizia mechi yake ya tatu Februari 26 ugenini dhidi ya Real Bamako.
LigiKuu Simba, Yanga zawajua wapinzani CAF
Simba, Yanga zawajua wapinzani CAF
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
