Na mwandishi wetu
Kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili amewaaga mashabiki wa timu hiyo kwa kueleza wazi kuwa anaondoka katika kikosi cha timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Kabwili pia ni kama vile ametegua kitendawili cha nini kinaendelea kuhusu hatma yake baada ya kutoonekana kwenye kikosi cha timu hiyo tangu Novemba mwaka jana na kuondoka kabisa kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Kigamboni.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kabwili alieleza kuhusiana na hilo, akiishukuru timu hiyo kwa kumfunza mengi na kumuamini katika nyakati zote na kwamba atawakumbuka daima.
“Nipende kumshukuru mwenyezi Mungu kwa muda wote wa miaka mitano niliotumikia Yanga SC, nasema ahsante na Mungu awabariki mtabaki kichwani mwangu daima. Nimejifunza mengi hasa kuamini kila nyakati za misimu bila kukata tamaa katika kazi yangu.
“Mmesaidia kunikomaza kwa hali zote za maisha yangu, leo najivunia kwa Watanzania, mashabiki, viongozi na wachezaji wenzangu mtabaki milele kichwani mwangu, asante Wananchi,” alieleza Kabwili aliyewahi kunolewa kwenye Akademi ya Azam.
Kabwili amedumu Yanga tangu mwaka 2017 aliposajiliwa na timu hiyo baada ya kuonesha kiwango kikubwa kwenye michuano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 iliyofanyika nchini Gabon.
Soka Kabwili awaaga mashabiki Yanga
Kabwili awaaga mashabiki Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
