Manchester, England
Mpango wa Man United kumsajili straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (pichani) bado upo vile vile na sasa klabu hiyo imeongeza wachezaji wengine wawili katika orodha ya wachezaji inaowataka.
Katika orodha hiyo mbali na Kane, wachezaji wengine ambao Man United inawataka ni pamoja na kiungo wa West Ham, Declan Rice na kiungo wa Chelsea, Mason Mount.
Man United tayari imejihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya jana Alhamisi kuilaza Chelsea mabao 4-1 na kujiimarisha katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag amenukuliwa akisema wamerudi katika mashindano ‘yanayowahusu’ lakini akatahadharisha umuhimu wa kufanyika uwekezaji na kuimarisha zaidi timu hiyo.
Inaaminika kwamba nia ya Ten Hag ni kumuunganisha Kane na Marcus Rashford ili kuiboresha zaidi safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini sasa amewaongeza katika hesabu zake Rice na Mount.
Huenda timu hiyo isipate wakati mgumu kuwasajili Rice na Mount lakini kazi huenda ikawa ngumu kwa Kane ambaye zipo habari kwamba pia anatakiwa na klabu kadhaa ikiwamo PSG ya Ufaransa.
Jambo zuri kwa Kane ni kwamba mwenyewe ameonesha nia ya kutaka kuihama timu hiyo kwa lengo la kusaka changamoto mpya nje ya Spurs, klabu ambayo amejijengea jina kubwa akiwa mshambuliaji tegemeo.
Kimataifa Kane, Rice, Mount watakiwa United
Kane, Rice, Mount watakiwa United
Read also