Na mwandishi wetu
Klabu ya Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC imeruhusiwa kuendelea na usajili wa wachezaji kama kawaida baada ya adhabu yao ya kutosajili kuondolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Tamko hilo limetolewa leo Ijumaa ikiwa ni siku mbili pekee zimepita tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze kufungiwa kwa timu hiyo pamoja na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship baada ya kocha Ahmed El Faramawy Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo alizowahi kuzinoa kwa nyakati tofauti.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameeleza kwamba kilichotokea ni kwamba Kitayosce imelipa fedha zote ilizokuwa ikidaiwa na kocha huyo raia wa Misri kwa klabu hiyo kumvunjia mkataba kinyume na taratibu.
“Ni uamuzi uliotolewa na Fifa baada ya Kitayosce kulipa madai yao yote kwa kocha Ahmed Soliman. Kwa hatua hiyo sasa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania nalo limeiondolea adhabu Kitayosce ya kutofanya usajili wa ndani,” alisema Ndimbo.
Soka Kitayosce sasa ruksa kusajili
Kitayosce sasa ruksa kusajili
Read also