Na mwandishi wetu
Timu ya Mlandege imefanikiwa kulitetea Kombe la Mapunduzi baada ya kuilaza Simba bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumamosi hii usiku kwenye dimba la New Amaan Complex.
Bao pekee lililoizamisha Simba katika mchezo huo lilipatikana dakika ya 54 mfungaji akiwa ni Joseph Akandwanao kwa shuti kali baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Simba
Simba licha ya kuutawala mchezo na kucheza kwa pasi za uhakika ilihaha kusaka bao la kusawazisha lakini ukuta mgumu wa Mlandege ulikuwa kikwazo hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Kwa ushindi huo, Mlandege wameondoka na kitita cha Sh milioni 100 wakati Simba walioshika nafasi ya pili wameondoka na kitita cha Sh 70 milioni.
Wakati Mlandege ikiweka rekodi ya kulibeba taji hilo kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2023, Simba wao wana rekodi ya kulibeba taji hilo mara tatu wakilibeba mwaka 2011, 2015 na 2022.
Soka Mlandege yabeba taji la Mapinduzi, yaizima Simba
Mlandege yabeba taji la Mapinduzi, yaizima Simba
Read also
