Porto, Ureno
Winga wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo amesema kwamba ataendelea kuichezea timu yake ya taifa licha ya kutolewa kwenye fainali za Euro 2024.
Ronaldo, 39, amekuwa akihusishwa na mipango ya kustaafu kuichezea timu hiyo ingawa hivi karibuni alisema kwamba fainali za Euro 2024 ni za mwisho kwake kwamba hatokuwamo kwenye fainali za 2028 ingawa hajasema lolote kuhusu fainali za Kombe la Dunia 2026 akiwa na miaka 41.
Kabla ya Ureno kutolewa kwenye fainali za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani, Ronaldo alicheza mechi tano za michuano hiyo akitumia wastani wa dakika 97 kwa kila mechi.
Safari hii hata hivyo Ronaldo aliweka rekodi mpya ya kutotoka na bao katika michuano mikubwa ya kimataifa na hivyo hadithi ya kustaafu kwake ikazidi kupamba moto.
Ronaldo ambaye pia ndiye nahodha wa timu ya Ureno mara baada ya timu hiyo kutolewa kwenye Euro 2024 na Ufaransa kwa penalti 5-3, alitumia mitandao ya kijamii kuonesha kwamba huo si mwisho wake.
“Tunahitaji zaidi, tunastahili zaidi, ni kwa ajili yetu na kwa kila mmoja wenu, kwa ajili ya Ureno,” alisema nyota huyo wa zamani wa timu za Man United na Real Madrid.
Kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Roberto MartÃnez mara baada ya timu yake kutolewa kwenye Euro 2024 alisema ni mapema mno kusema kwamba Ronaldo amecheza mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa lake.
Ronaldo alianza kuichezea timu ya Ureno mwaka 2003 na anashikilia rekodi ya kipekee akiwa ameifungia mabao 130 katika mechi 212, mwaka 2016 aliiwezesha kubeba taji la Euro 2016, michuano ambayo pia ameiwakilisha nchi yake katika fainali sita tofauti.
Kimataifa Ronaldo hana mpango kustaafu
Ronaldo hana mpango kustaafu
Read also
