Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Heri Sasii kuwa mwamuzi wa mechi ya Ngao ya Jamii inayosubiriwa kwa hamu baina ya Yanga dhidi ya Simba itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo maarufu Dar Derby au Kariakoo Derby ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC wa 2022/23 imeteka hisia za mashabiki wengi kutokana na usajili uliofanywa na timu hizo na tambo za viongozi wa klabu hizo.
Sasii mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) atakuwa na wasaidizi wake, Kassim Mpanga na Mohamed Mkono wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Ramadhan Kayoko, mtathimini wa mchezo ni Nassor Hamduni.
Kwa mujibu wa kanuni mechi hiyo huwakutanisha bingwa wa Ligi Kuu na bingwa wa Kombe la Azam (ASFC) lakini kwa kuwa Yanga ni bingwa wa michuano yote hiyo, inalazimika kupepetana na timu iliyoshika nafasi ya pili kwenye ligi msimu uliopita ambao ni Simba.
Soka Heri kupuliza filimbi Dar Derby
Heri kupuliza filimbi Dar Derby
Read also