Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji wa kimataifa na wa ndani.
Mashirikisho hayo yamefikia uamuzi huo baada ya aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Lazarus Kambole (pichani juu) kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo kuhusu kutolipwa haki zake na klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na TFF Jumanne hii, taarifa hiyo imeeleza kuwa Kambole aliishitaki Yanga kwa madai ya malimbikizo ya mshahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba.
Katika madai hayo, timu hiyo ilipewa siku 45 kulipa pesa hizo na ilishindwa ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa kushindwa kutekeleza hukumu ndani ya muda husika ndio sababu ya timu hiyo kufungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa ndani na wa nje.
Yanga ilimtambulisha Kambole raia wa Zambia Juni 16, mwaka juzi akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Septemba, mwaka huo huo iliachana na mchezaji huyo na kumpeleka kwa mkopo kwenye timu ya Wakiso Giant ya Uganda.
Soka Fifa yaifungia Yanga kusajili
Fifa yaifungia Yanga kusajili
Related posts
Read also