Manchester, England
Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amesema anatarajia winga, Cristiano Ronaldo atabaki katika timu hiyo na kwamba hawatanunua mchezaji mwingine yeyote mara baada ya kukamilisha usajili wa Antony na Martin Dubravka.
Man Utd imekubali kulipa ada ya Pauni 81.3 milioni kwa ajili ya kumsajili winga Mbrazil, Antony kutoka Ajax wakati huo huo wakiwa katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha usajili wa kipa Dubravka wa Newcastle United.
“Kwa dirisha hili la usajili huo utakuwa ndio mwisho kwetu, kwa klabu kubwa wakati wote unatakiwa kuwa tayari kwa lolote lakini kimsingi ni kwamba tutakwenda na kikosi hiki kuanzia Septemba hadi Januari,” alisema Ten Hag kuhusu dirisha la usajili ambalo linafungwa rasmi kesho Alhamisi.
Ten Hag pia hakutaka kumzungumzia sana Antony na siku atakayowasili katika klabu hiyo kwa alichodai kwamba kuna mambo ambayo hayajakamilika na yanaendelea kufanyiwa kazi ingawa aliweka wazi nia ya klabu hiyo kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Alipoulizwa kuhusu Ronaldo, Ten Hag alisema, “Ni jambo lililo wazi kwamba tunahitaji wachezaji wa hadhi, unahitaji wachezaji zaidi kwa ajili ya mechi zote ili kuwa na mwendelezo, hicho ndicho tunachokipigania kwa sasa.”
Ronaldo ambaye msimu uliopita ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa Man Utd akiwa na mabao 24 katika mashindano yote, amekuwa akidai kutaka kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi hiki cha kiangazi ingawa hivi karibuni alisema ataweka wazi ukweli kuhusu mambo yake yajayo baada ya kusoma habari nyingi za uwongo katika kipindi cha dirisha la usajili.
Kimataifa Ten Hag afunga usajili, ambakisha Ronaldo
Ten Hag afunga usajili, ambakisha Ronaldo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
