Na mwandishi wetu
Timu ya Pazi inatarajiwa kufungua pazia la mashindano ya kikapu ya East Division ya BAL kwa kucheza na Elan Cotton BBC ya Benin katika Uwanja wa Ndani wa Shule ya Sekondari ya Kimataifa (IST), Dar es Salaam.
Mashindano hayo ambayo yanaanza kesho Alhamisi na kumalizika Oktoba 21, yanashirikisha timu nne kutoka Burundi, Kenya, Benin na Tanzania ambazo zinapambana kupata nafasi moja ya kuwakilisha Kundi C – East Division kwenye Michuano ya Elite 16 ya BAL mwakani.
Timu hizo ni Dynamo (Burundi), KPA (Kenya), Elan Cotton na Pazi ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Kadebe alitoa hamasa kwa mashabiki wa Tanzania kwenda kuishangilia Pazi ambao ni mabingwa wa taifa huku ikiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.
“Njooni mashabiki muishabikie Pazi ikiwa ni timu pekee inayoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya BAL. Pazi ikishinda, Tanzania imeshinda,” alisema.
Kikapu Pazi kufungua pazia East Division
Pazi kufungua pazia East Division
Read also