Madrid, Hispania
Kocha wa PSG, Luis Enrique huenda akalazimika kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka timu hiyo ianze mapema kujipanga bila ya Kylian Mbappe baada ya mshambuliaji huyo kufunga mabao mawili na kuiwezesha PSG kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Enrique alitangaza mpango huo na kuanza kuufanyia kazi katika mechi mbili za Ligi 1 dhidi ya Rennes na dhidi ya Monaco, alimuweka benchi Mbappe baada ya kucheza kwa dakika kadhaa na mechi zote hizo ziliisha kwa sare.
Mabao mawili ya Mbappe aliyofunga jana Jumanne usiku dhidi ya Real Sociedad yameifanya PSG kutoka uwanjani na ushindi wa 2-1 na kufuzu robo fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-1, mabao hayo yanatosha kabisa kumfikirisha upya Enrique, bao pekee la Sociedad lilifungwa na Merino.
Si Enrique pekee, hata mabosi PSG nao wana kazi ya kutafakari kama ni sahihi kumuachia Mbappe aondoke licha ya ukweli kwamba mkataba wake unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu na habari zilizopo ni kwamba mazungumzo yake na Real Madrid yanakwenda vizuri.
Kutokana na juhudi hizo za Mbappe, PSG sasa wanasubiri hapo Machi 15 ili kumjua mpinzani wao katika mechi ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa ya klabu barani Ulaya..
Nayo Bayern Munich, timu ambayo imekuwa na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Ujerumani au Bundesliga, jana ilifanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuilaza Lazio mabao 3-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo nyota ya nahodha wa England, Harry Kane iling’ara baada ya kutupia wavuni mabao mawili peke yake wakati bao la tatu likifungwa na Muller.
Matokeo ya mechi za jana Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Bayern Munich 3-0 Lazio
Real Sociedad 1-2 PSG
Kimataifa Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya
Mbappe aipeleka PSG robo fainali Ulaya
Read also