London, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amesema anajua kilichotokea lakini hataki kuelezea tukio la Erling Haaland na Kyle Walker kuzozana na maofisa wa Arsenal baada ya mechi baina ya timu hizo iliyoisha kwa City kulala kwa bao 1-0.
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika jana Jumapili kwenye dimba la Emirates, Walker na Haaland walijikuta wakizozana na mmoja wa makocha wa Arsenal, Nicolas Jover ambaye siku za nyuma alikuwa kocha Man City.
“Najua nini kilichotokea lakini sisemi lolote, wao Arsenal wanajua kila kitu,” alisema Pep akizungumzia tukio hilo lililojitokeza mara baada ya mechi hiyo ya Ligi Kuu England (EPL).
Gabriel Martinelli ndiye aliyefunga bao pekee la Arsenal lililoipa timu hiyo ushindi dhidi ya City ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo.
Tukio hilo lilitokea wakati wachezaji wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lakini ghafla Walker alimgeukia Jover na kuanza kuzozana naye na hapo hapo Haaland akaingilia kati kumtetea mchezaji huyo kabla ya maofisa wa klabu zote kuingilia na kuanza kuamua ugomvi ulioanza kuibuka.
Utata huo uliendelea wakati wachezaji wakitoka uwanjani ambapo baadaye Bukayo Saka akaingilia kati na kumuondoa Jover katika tukio hilo.
Jover alikuwa mmoja wa makocha wasaidizi wa Man City kati ya mwaka 2019 hadi 2021 alipoamua kuungana na kocha Mikel Arteta katika klabu ya Arsenal.
Matokeo ya mechi za EPL wikiendi ni kama ifuatavyo…
Brighton 2-2 Liverpool
West Ham 2-2 Newcastle
Wolves 1-1 Aston Villa
Arsenal 1-0 Man City
Luton Town 0-1 Tottenham
Burnley 1-4 Chelsea
Everton 3-0 Bournemouth
Fulham 3-1Sheffield United
Man United 2-1 Brentford
Crystal Palace 0-0 Nottingham
Kimataifa Pep akataa kuzungumzia ugomvi
Pep akataa kuzungumzia ugomvi
Read also