Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwapa muda wachezaji wapya waliowasajili kwenye dirisha dogo wakiwemo washambuliaji Pa Omar Jobe na Freddy Michael Kouablan.
Jobe na Kouablan wamejiunga na miamba hiyo ya soka kuziba nafasi ya Jean Baleke na Moses Phiri na juzi walianza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) FA na kuonesha kiwango cha wastani.
Kocha huyo alisema wachezaji hao wana uwezo mkubwa wa kucheza na kufunga lakini wanahitaji kuzoeana na wenzao kabla ya kufanya kile ambacho mashabiki wanatarajia kukiona kutoka kwao.
“Ni wachezaji wa daraja la juu ndio maana nikapendekeza wasajiliwe, naamini wataifanyia Simba kitu kikubwa katika mashindano yote tunayoshiriki, kitu cha msingi ni vyema mashabiki wakawapa muda ili waweze kuzoea mazingira,” alisema Benchikha.
Kocha huyo raia wa Algeria alisema kutokana na malengo waliyonayo ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki atahakikisha anawafua wachezaji hao na kuendana na mifumo ya timu haraka iwezekanavyo.
Benchikha PIA amepongeza uwezo uliooneshwa na wachezaji wapya wazawa waliosajiliwa dirisha dogo wakiwemo Ladack Chasambi, Edwin Balau na Salehe Karabaka na kueleza kuwa wanatoa upinzani mkubwa kutokana na ubora na kasi waliyonayo uwanjani.
Soka Benchikha awakingia kifua wachezaji wapya
Benchikha awakingia kifua wachezaji wapya
Read also