Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Geita Gold FC, Denis Kitambi amesema bado ana imani na kikosi chake licha ya kupoteza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu NBC.
Akizungumza na GreenSports, Kitambi alisema mifumo mipya ya uchezaji na makosa madogomadogo yanayofanywa na wachezaji wake ndivyo vilichangia wapoteze mechi hizo lakini anafurahi kuona kuna mabadiliko makubwa ya uchezaji kwenye timu yake.
“Ni kweli hatujafanya vizuri kwenye mechi tatu zilizopita, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kushuka daraja, bado tuna mechi nyingi za kurekebisha makosa yetu, tatizo letu ni kubadili mifumo ya uchezaji ambayo pia vijana wangu wameanza kuizoea,” alisema Kitambi.
Alisema kuwa uimara walionao hivi sasa unampa matumaini ya kufanya vizuri mechi zinazofuata za ligi na itawaongezea ari ya kufanya vizuri wachezaji wake.
Vipigo hivyo ambavyo ni dhidi ya Simba kwa bao 1-0 kisha Azam mabao 2-1 kabla ya kufungwa na Ihefu mabao 2-1 pia, vimeiweka Geita katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Geita Gold kwa mwendo ilionao kwenye ligi hadi sasa imekusanya jumla ya pointi 16 katika idadi kama hiyo ya mechi walizocheza.
Soka Kitambi ajipa matumaini Geita
Kitambi ajipa matumaini Geita
Read also