Barcelona, Hispania
Rais wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta amekanusha uvumi ulionea kwamba klabu yake italazimika kumruhusu nyota wake Frenkie de Jong anayewindwa na Man United aondoke katika kipindi hiki ili kukidhi matakwa ya kanuni ya matumizi sahihi ya fedha katika soka.
Kwa kipindi kirefu Man United imekuwa ikionyesha shauku ya kumtaka mcheaji huyo kwa ada inayotajwa kufikia Euro 85 milioni lakini habari za ndani zinadai kuwa kiungo huyo Mholanzi anapendelea zaidi kubaki Barca.
Kuondoka kwa De Jong kunatajwa kuwa kutaisaidia Barca kupunguza malipo makubwa ya mishahara na hatimaye kuwa na uwezo wa kuwasajili beki wa kulia, Sergi Roberto pamoja na kumudu gharama za wachezaji Franck Kessie na Andreas Christensen.
Laporta hata hivyo akizungumza Ijumaa hii wakati wa kutambulisha usajili mpya wa Raphinha ambaye amejiunga na Barca akitokea Leeds United, alisema klabu yake inaweza kumzuia De Jong asiondoke.
“Si kweli kwamba klabu inalazimika kumuuza Frenkie de Jong,” alisema Laporta licha ya kuwapo habari kwamba klabu hiyo inakabiliwa na hali ngumu kifedha.
Sambamba na hilo, Laporta pia alithibitisha kwamba De Jong atakuwamo katika msafara wa wachezaji wa timu hiyo ambao kesho Jumamosi watasafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.
Wakati huo huo, Barcelona bado haijakata tamaa katika mbio zake za kumpata mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ambaye klabu hiyo haitaki kumuachia licha ya mchezaji mwenyewe kudai kwamba anataka kuondoka.
“Hatujapata jibu lolote kutoka Bayern lakini siwezi kuzungumza suala hilo kwa undani na kuikosea heshima Bayern,” alisema Laporta.
Kimataifa Laporta: Hatulazimiki kumuuza De Jong
Laporta: Hatulazimiki kumuuza De Jong
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
