Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuomba nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba awe balozi wa nchi hiyo kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027.
Fainali za Afcon 2027 zitafanyika nchini Tanzania kuanzia Juni mwakani, nchi hiyo itakuwa mwenyeji ikishirikiana na majirani zake wa Kenya na Uganda
Kauli Rais Samia imekuja baada ya wawili hao kufanya mazungumzo Jumanne Mei 5, 2026 Ikulu ya Dodoma muda mfupi baada ya mchezaji huyo ambaye pia alitamba na timu ya taifa ya Ivory Coast kuwasili mjini humo.
Rais Samia pia aliitaka Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Drogba na kuutumia uzoefu wake katika michezo ikiwamo uanzishwaji wa akademi kama njia mojawapo ya kukuza michezo nchini.
Kwa upande wake Drogba alimshukuru Rais Samia kwa mualiko huo na kuahidi kushirikiana na Tanzania katika suala zima la kuendeleza michezo.
Drogba alijipatia umaarufu zaidi kwenye soka hasa miaka ya 2000 ambapo akiwa na klabu ya Chelsea alibeba taji la Ligi Kuu England mara kadhaa, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kushinda tuzo ya mfungaji bora.
Sambamba na hilo, Drogba pia amekuwa na mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Ivory Coast na kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali ya kijamii nchini humo.
Baada ya kustaafu soka aliingia katika kinyang’anyiro cha kuusaka uongozi kwenye Shirikisho la Soka Ivory Coast ingawa mpango huo haukufanikiwa.
Kimataifa Rais Samia amuomba Drogba awe balozi Afcon
Rais Samia amuomba Drogba awe balozi Afcon
Read also
