Na mwandishi wetu
Baada ya Yanga jana kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu hiyo huku akiitakia kila la heri kuelekea hatua inayofuata.
Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye Mtandao wa Kijamii wa Twitter, Rais Samia aliandika: “Kongole Yanga kwa ushindi na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka la wanaume kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, nawatakia kila la heri kwenye hatua inayofuata.”
Mbali na Rais Samia pia Rais wa Heshima wa Simba SC na mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ naye ameipongeza Yanga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania huku akiwakaribisha kwenye michuano ya ngazi ya klabu Afrika.
Yanga ilifanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo ambayo mara ya mwisho waliingia msimu wa 2015-16 kwa kuifumua bao 1-0 Club Africain ya Tunisia baada ya suluhu ya mechi ya awali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Wanajangwani hao walilazimika kucheza hatua ya mtoano na Africain baada ya kufungwa jumla ya mabao 2-1 na Al Hilal ya Sudan na hivyo kudondokea kwenye mechi za kuwania kufuzu kushiriki makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa inasubiri droo itakayopangwa Novemba 16, mwaka huu mjini Cairo, Misri kujua itacheza na timu gani hatua ya makundi.
Soka Rais Samia aipongeza Yanga
Rais Samia aipongeza Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
