Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amesema sare ya 0-0 waliyoipata jana Ijumaa dhidi ya Asec Mimosas katika Ligi ya Mabingwa Afrika haijapunguza ari yao ya kutinga robo fainali.
Jumamosi ijayo Simba itamaliza mechi za makundi kwa kucheza na Jwaneng Galaxy, na endapo itashinda itafikisha pointi tisa na kufuzu kama mshindi wa pili kwenye Kundi B nyuma ya Asec Mimosas yenye pointi 11.
“Nawapongeza sana wachezaji wangu, walicheza kwa kujituma kuipambanaia nembo ya Simba hasa kipindi cha pili ambacho tulitengeneza nafasi nyingi lakini tulishindwa kufunga lakini hiyo haijatukatisha tamaa, imetuongezea ari ya kupambana kutinga robo fainali,” alisema Benchikha.
Alisema uwezo huo wanao na hiyo ni kutokana na mchezo huo kuchezwa nyumbani Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo watakuwa mbele ya mashabiki zao.
Kocha Mkuu wa Asec, Juliet Chevalier alisema: “Simba walitupa presha, mara kadhaa walikaribia kufunga lakini naipongeza safu yangu ya ulinzi, ilifanya kazi nzuri kiujumla na mchezo ulikuwa mzuri lakini malengo yetu ilikuwa ni kushinda mchezo huu ili kutengeneza rekodi nzuri kwetu,” alisema Chevalier.
Kimataifa Benchikha aamini Simba itafuzu robo fainali
Benchikha aamini Simba itafuzu robo fainali
Read also
