Na mwandishi wetu
Uongozi wa Namungo umetangaza kuachana na kocha wao, Denis Kitambi na kumshukuru kwa ushirikiano wake katika muda wote aliodumu na timu hiyo.
Namungo imeeleza hayo leo Jumatano kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo imeandika: “Uongozi wa Namungo FC unapenda kumshukuru Kocha Denis Kitambi kwa muda wote aliotumikia timu kwa ushirikiano mkubwa ndani ya timu yetu.”
Kitambi anakuwa kocha wa pili kuondoka Namungo msimu huu baada ya Cedric Kaze aliyejiuzulu Oktoba 22, mwaka huu baada ya kuiongoza Namungo katika mechi sita za awali bila ya ushindi.
Kitambi anaondoka Namungo baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi saba ambapo ilishinda mechi nne, sare mbili na kufungwa moja.
Hata hivyo, tetesi zinaeleza kuwa kocha huyo yuko mbioni kutua Geita Gold kuchukua nafasi ya Hemed Morocco ambaye anaonekana kuwa na matokeo ya kusuasua kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya 14 ikiwa imeshinda mechi tatu, sare nne na kufungwa mara tano.
Soka Namungo yaachana na Kitambi
Namungo yaachana na Kitambi
Read also