Na mwandishi wetu
Rais wa Klabu ya Yanga, Hersi Said ameeleza kwamba anajua wao kama viongozi wana jukumu zito la kuhakikisha wanapambana kupata matokeo kwenye mechi yao dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Yanga inahitaji matokeo ya ushindi au sare ya kuanzia 2-2 ili wasonge kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi ya awali iliyopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuisha kwa sare ya bao 1-1.
“Wanachama, wapenzi wa Yanga wanapenda timu yao iendelee hatua inayofuata ya makundi, viongozi wa Serikali, imesikika kauli ya Waziri (Mohamed Mchangerwa, Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo) inatupa maelekezo hayo ya kupambana kufuzu Sudan, tunaamini timu itafanya vizuri.
“Tunatarajia timu yetu ivuke kwenda hatua ya makundi na hayo ndiyo malengo yetu, tunapeleka ujumbe huu pia kwa wachezaji, benchi la ufundi wajue kwamba kuna mahitaji makubwa nyuma yao na naamini timu yetu itakwenda kufanya vizuri,” alisema Hersi.
Yanga inatarajia kukwea pipa Ijumaa ya keshokutwa kuifuata Hilal kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Jumapili hii, majira ya saa tatu usiku kwenye Uwanja wa Al Hilal, Khartoum.
Soka Hersi: Tuna jukumu zito Sudan
Hersi: Tuna jukumu zito Sudan
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
