London, England
Kiungo wa Arsenal, Declan Rice amefurahia kupewa nafasi ya kuwa nahodha wa timu ya England katika mechi ya leo Jumanne dhidi ya Ubelgiji ambayo pia inakuwa mechi yake ya 50 na timu hiyo.
Rice, 25, amekuwa mchezaji muhimu England tangu apate nafasi ya kuichezea timu hiyo mara ya kwanza mwaka 2019 na leo kwenye dimba la Wembley atakuwa nahodha katika mechi hiyo ya kirafiki.
Mchezaji huyo amepewa nafasi hiyo baada ya nahodha mkuu Harry Kane na msaidizi wake, Kyle Walker kuwa majeruhi na hivyo hawatakuwamo katika kikosi cha England kwenye mechi ya leo.
“Mechi yangu ya 50 nakwenda kwenye dimba la Wembley mbele ya familia yangu na marafiki, ni heshima kubwa, najikuta sina la kusema,” alisema Rice.
Tukio la Rice kupewa unahodha katika mechi yake ya 50 linaweza pia kumkumbusha miaka mitano iliyopita alipopata nafasi ya kuichezea England kwa mara ya kwanza dhidi ya Jamhuri ya Czech mwaka 2019 na sasa anajivunia kuifikisha timu hiyo kwenye hatua ya fainali ya Euro 2020 na robo fainali ya Kombe la Dunia 2022.
“Nimepiga hatua kubwa kiuchezaji, na kama binadamu tangu nije katika kundi hili kwa mara ya kwanza, kadri muda ulivyokwenda nimeweza kucheza mechi kubwa zaidi za michuano mikubwa, nimekuwa nikifurahia kila hatua,” alisema Rice.
Kikosi cha England chini ya kocha Gareth Southgate kinaandamwa na janga la majeruhi ambapo mbali na Walker na Kane, wengine ni Bukayo Saka, Luke Shaw, Harry Maguire, Sam Johnstone na Trent Alexander-Alexander.
Mechi za kimataifa za kirafiki leo Jumanne Machi 26, 2024
England v Ubelgiji
Uganda v Ghana
Finland v Estonia
Latvia v Liechtenstein
Hungary v Kosovo
Malta v Belarus
Norway v Slovakia
Jamhuri ya Czech v Armenia
Colombia v Romania
Ivory Coast v Uruguay
Senegal v Benin
Austria v Uturuki
Ujerumani v Uholanzi
Luxembourg v Kazakhstan
Jamhuri ya Ireland v Uswisi
Scotland v Ireland Kask
Slovenia v Ureno
Misri v Croatia
Ufaransa v Chile
Mali v Nigeria
New Zealand v Tunisia
Hispania v Brazil
Algeria v Afrika Kusini
Morocco v Mauritania