Na mwandishi wetu
Azam haijapoa, leo imemtambulisha kiungo mshambuliaji mwingine Cleophas Mkandala kutoka Dodoma Jiji ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Mkandala ambaye msimu huu uliopita wa 2021/22 ameonesha kiwango kizuri akiwa na Walima Zabibu, kwenye kandarasi yake kuna kipengele cha kuongeza mkataba wa miezi sita na klabu hiyo ikitegemeana na kiwango atakachokionesha mchezaji huyo wa zamani wa Tanzania Prisons ya Mbeya.
Usajili huo uliotambulishwa leo unakuwa wa nne kwa Azam tangu ilipoanza kutangaza silaha zake nne lakini unakuwa wa kwanza kwa wachezaji wazawa.
Wengine waliotambulishwa na Azam mpaka sasa mbele ya mmiliki wa timu hiyo, Yusuf Bakhresa na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ni kiungo mkabaji wa Nigeria, Issa Ndala na viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho raia wa Ivory Coast.
Soka Azam yasajili kiungo Dom Jiji
Azam yasajili kiungo Dom Jiji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
