Na mwandishi wetu
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema wamelazimika kwenda nchini Morocco ili kuipa timu muda wa kutosha kuizoea hali ya hewa na kupata muda wa siku mbili za kufanya mazoezi kabla ya kuikabili Wydad AC.
Simba inaingia kuikabili Wydad ikiwa na mtaji wa bao 1-0, ushindi walioupata wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na sasa inatafuta angalau sare ugenini, ipenye hatua ya nusu fainali.
Kajula alisema wameenda Moroco wakiwa na tahadhari kubwa kwa sababu sio mechi rahisi lakini wanaamini wana kikosi bora ambacho kipo kwenye kwenye kiwango bora na imani yao wanaweza kufanya vizuri na kuibuka na ushindi.
“Tuna wachezaji wazoefu wa kucheza michezo mikubwa na uzuri wa kucheza mechi nyingi za kimataifa zinajenga hali ya kujiamini lakini hatupaswi kujiamini kupita kiasi ni shida, tunaamini tuna timu ambayo imejiandaa vizuri kuelekea kwenye mechi inayofuata,” alisema.
“Timu ya mpira imegawanyika kwenye maeneo tofauti, viongozi kazi yetu ni kuhakikisha wachezaji wanasafiri wanapata mahitaji ya msingi hawakwami wanawahi kufika,” alisema Kajula.
Alisema Simba si timu ya kuagua au kueleza kitu ambacho si cha kimpira, wanaamini kwenye matokeo ya uwanjani, wamefanya maandalizi mazuri kuelekea kwenye mechi hii lakini pia wanatambua Wydad ni timu bora ambaye ni bingwa mtetezi hivyo wamejipanga kukabiliana naye kwao.
Simba imefika jana nchini Morocco wakiwa wameanza safari yao siku mbili baada ya mechi yao ya awali iliyopigwa Jumamosi iliyopita. Wekundu hao watavaana na Wydad Ijumaa hii kwenye Uwanja wa Mohamed V, Casablanca.
Kimataifa Simba yataja sababu za kuwahi Morocco
Simba yataja sababu za kuwahi Morocco
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
