Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kwamba timu yake inatakiwa kuutafuta ubora wa moja kwa moja ili iwemo kwenye Top Four katika Ligi Kuu England (EPL).
Klopp ametoa kauli hiyo baada ya timu yake ikiwa nyumbani Anfield jana kukubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Leeds, ushindi ambao Leeds iliupata kwa bao la dakika ya 89 lililofungwa na Summerville na kubadili matokeo ya muda mrefu ya mchezo huo ya sare ya bao 1-1.
Leeds katika mechi hiyo ndio waliotangulia kupata bao dakika ya nne ya mchezo, mfungaji akiwa ni Rodrigo lakini dakika 10 baadaye mshambuliaji nyota wa Liverpool, Mohamed Salah alisawazisha bao hilo lakini mambo yaliharibika dakika moja kabla ya mpira kumalizika na Liverpool kujikuta ikipoteza pointi zote tatu huku Leeds ikijinasua kwenye janga la kushuka daraja.
Ushindi ambao Liverpool iliupata dhidi ya Man City uliibua matumaini mapya lakini kwa hali ilivyo ni kama vile bado timu hiyo haijawa katika ubora wake hasa baada ya kushindwa kutamba mbele ya timu zinazoonekana kuwa ni dhaifu za Nottingham Forest na sasa Leeds na sasa timu hiyo inashika nafasi ta tisa kwenye EPL ikiwa na pinti 16.
“Huwezi kufuzu Ligi ya Mabingwa kama uchezaji si wa katika ubora endelevu kama ambavyo tunafanya sasa, ni lazima tujiweke sawa katika hilo,” alisema Klopp ambaye katikati ya wiki iliyopita timu yake imetoka kupata ushindi mnono wa mabao 3-0 mbele ya Ajax kwenye Ligi ya Mabingwa na ilitegemewa kasi hiyo ingeendelezwa kwenye EPL.
“Kuna mambo mengi ambayo hayakubaliki likiwamo hili, samahani hiyo ndiyo hali ilivyo, sina hakika tutazama kulifanyia kazi hili kwa kiasi gani lakini tunatakiwa kufanya hivyo na ni lazima tufanye kazi ya kutafuta suluhisho, tunalazimika kuiangalia mechi hii kwanza na kujaribu kuielewa kwa undani kidogo na baadaye kujua nini cha kufanya kuanzia hapo,” alisema Klopp.
Kimataifa Klopp ahofu kuikosa Top Four
Klopp ahofu kuikosa Top Four
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
