London, England
Nahodha wa Man City, Ilkay Gundogan huenda akaihama timu hiyo baada ya kutakiwa na timu nne tofuati ingawa kocha Pep Guardiola anaamini msimu ujao atakuwa na mchezaji huyo Man City.
Gundogan (pichani) ambaye ana umri wa miaka 32 huenda akarudi Borussia Dortmund ambayo imeonesha nia ya kumtaka hasa baada ya Barcelona ambayo pia inamtaka kukwamishwa na suala la mshahara wa mchezaji huyo.
Ukiachana na klabu hizo mbili ambazo kila moja inamchungulia mwenzake, Arsenal nayo ipo tayari kumpa mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili na marupurupu ya maana hapo hapo kukiwa na habari kwamba kuna klabu ya Saudi Arabia nayo inamtaka.
Gundogan anaonekana kutaka mkataba mrefu katika klabu hizo jambo ambalo linazifanya zote zisite kutokana na umri wake hapo hapo zikiwa zinaviziana katika kupanda dau.
Wakati yote hayo yakiendelea, Pep anaamini mchezaji huyo ataongeza mkataba Man City na kwamba timu hiyo itapenda kuendelea kuwa naye msimu ujao kutokana na umuhimu wake.
Pep anaamini kuwa mbali na umuhimu wa Gundogan uwanjani lakini pia mchezaji huyo ni kiongozi mzuri kwenye timu ambaye anasikilizwa na wachezaji wenzake na kwa hilo Pep hatopenda kuona akiondoka.
Kimataifa Timu nne zamtaka Gundogan
Timu nne zamtaka Gundogan
Read also
