Liverpool, England
Klabu mahasimu Liverpool na Everton zimeingia matatani na sasa zinasubiri kuadhibiwa kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wao kuingia katika ugomvi katika mechi baina ya timu hizo Jumatatu iliyopita.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Anfield na Liverpool kutoka na ushindi wa mabao 2-0, katika dakika ya 86 kulitokea mzozo kiasi cha baadhi ya wachezaji kushikana mashati.
Taarifa ya Chama cha Soka England (FA) ilieleza kuwa klabu zote zilishindwa kuwaongoza wachezaji wao katika namna ambayo wangejizuia kufanya matendo yasiyofaa michezoni badala yake hadi wachezaji wa akiba waliingia uwanjani na kuanza kukabiliana.
Andrew Robertson na kipa wa Everton Jordan Pickford walipishana kauli kwa kujibizana baada ya Robertson kuupiga mpira mbali. Wachezaji hao kila mmoja alipewa kadi za njano.
FA imezitaka klabu za Liverpool na Everton ambazo ni mahasimu wa kihistoria, hadi Februari 20 kila moja iwe imejibu hoja hizo.
Kimataifa Liverpool, Everton matatani
Liverpool, Everton matatani
Read also