Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17 (U17), Bakari Shime (pichani) ameita wachezaji 23 watakaoingia kambini Septemba 5, mwaka huu kujiandaa na mchezo dhidi ya Morocco.
Akizungumza kwa njia ya mtandao akiwa Uganda, Shime alisema ameita wachezaji hao kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
“Kalenda ya Fifa siku hizi inahusisha pia timu za wanawake hivyo kikosi hiki kitacheza na Morocco kwenye tarehe hizo za mechi kimataifa,” alisema Shime.
Wachezaji walioitwa ni Mariam Shaban wa Bunda Queen, Sarah Joel (Fountain Gate), Melikua Wiliam (Bunda Queen), Masika Khamis (Alliance Girls), Kurwa Rocket (Bunda Queen), Judith Magoti (JKT Queens), Winnifrida Casto (Oysterbay Queens).
Pia wamo Ester Maseke (Bunda Queen), Sabina Alex (Geita Gold Queens), Jamila Rajab (JKT Queens), Semeni Juma (Bunda Queen), Winifrida Gerald (JKT Queens), Mikaela Daffo (Billo Queens), Lydia Maximillian (TSC Queens), Naomi Samwel (Geita Gold Queens).
Wengine ni Mwatima Mwarabu (Ziba sekondari, Tabora), Yasinta Mitoga (Mkwawa Queens, Sara Lucas (Bunda Queens), Winfrida Charles (Alliance Girls), Mwanaidi Maulid (TSC Queens), Salome Sant (Mapinduzi Queens), Mariam Siyame (Fountain Gate) na Edna Makamba (Oysterbay Queens).