Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Ibrahim Ajibu amesema anaamini timu hiyo itafanya vizuri msimu ujao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na wachezaji wengi wazoefu waliopo hapo.
Akizungumza na GreenSports, Ajibu alisema ingawa timu hiyo ndiyo mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lakini ana imani watafanya vizuri kutokana na mipango ya timu ilivyo kuelekea mashindano hayo.
“Singida ni timu nzuri sababu ina wachezaji wengi wazuri na wazoefu, na mashindano yale yanahitaji sana uzoefu kwa hiyo wachezaji wengi waliopo hapa wameshacheza michuano hiyo kwa hiyo timu ndiyo itakuwa ngeni lakini wachezaji hawatakuwa wageni hivyo naamini itafanya vizuri,” alisema Ajibu.
Singida iliyoshiriki Ligi Kuu NBC kwa mara ya kwanza msimu huu, imemaliza kwenye nafasi ya nne na kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho msimu ujao.
Baadhi ya wachezaji waliopo Singida ambao wamewahi kushiriki michuano ya CAF ni pamoja na Meddie Kagere, Paschal Wawa, Francis Kazadi, Said Ndemla, Bruno Gomes na wengine.
Soka Ajibu: Singida Fountain itatamba Shirikisho
Ajibu: Singida Fountain itatamba Shirikisho
Read also