Oslo, Norway
Timu ya Arsenal imepiga hatua muhimu kuelekea kufuzu hatua ya mtoano ya Europa Ligi baada ya kuichapa Bodo-Glimt ya Norway kwa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa jana Alhamisi usiku.
Arsenal iliyokuwa ugenini ilifaidika na bao hilo pekee la Bukayo Sako aliyeshirikiana vizuri na kiungo Albert Sambi Lokonga kuipa ushindi timu hiyo dhidi ya timu inayojivunia rekodi nzuri ya kutopoteza mechi 14 mfululizo za nyumbani katika michuano ya Ulaya. Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa kwenye dimba la Emirates, Arsenal ikiwa nyumbani iliichapa timu hiyo mabao 3-0.
Ushindi wa jana unaifanya Arsenal iwe juu kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Bodo inayoshika nafasi ya tatu katika Kundi A ingawa Arsenal bado ina mechi moja mkononi baada ya mechi na PSV kuahirishwa kutokana na msiba wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.
PSV inayoshika nafasi ya pili sasa itacheza na Arsenal Alhamisi ijayo ambapo ushindi utaihakikishia moja kwa moja Arsenal tiketi ya hatua ya mtoano. Timu nyingine ya nne katika kundi hilo ni FC Zurich.
Ushindi huo japo mdogo unatosha kuwa sababu ya kumfurahisha kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kwani unatoa ishara njema ya mbio za timu hiyo kutamba Ulaya baada ya mwenendo mzuri kwenye Ligi Kuu England.
Matokeo mechi za Alhamisi Europa Ligi…
Bodø-Glimt 0-1 Arsenal
Man Utd 1-0 Omonia Nicosia
AEK Larnaca 1-2 Fenerbahce
Dynamo Kyiv 0-1 Rennes
Real Betis 1-1 Roma
Saint-Gilloise 3-3 Sporting Braga
Feyenoord 2-2 FC Midtjylland
FK Qarabag 0-0 Olympiakos
Nantes 0-4 Freiburg
PSV Eindhoven 5-0 Zürich
Ludogorets 2-0 HJK Helsinki
Union Berlin 1-0 Malmö FF
Kimataifa Arsenal yajiweka pazuri Europa Ligi
Arsenal yajiweka pazuri Europa Ligi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
