Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imetangaza kuunda kamati maalum ya kusimamia mchakato wa marekebisho ya katiba ya klabu hiyo sambamba na kutaja tarehe ya mkutano mkuu kwa mwaka huu utakaofanyika Januari 21, mwakani.
Taarifa hiyo iliyotolewa leo Ijumaa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kupitia mtandao wa klabu hiyo imefafanua kuwa mabadiliko hayo ni kulingana na muktadha wa maelekezo kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na maoni ya wanachama.
Kamati hiyo inaundwa na Wakili Hussein Mlinga (mwenyekiti), Wakili Aziza Msangi (makamu) na Ustadhi Masoud, Zulfika Chandoo, Moses Kaluwa, Hamis Mkomwa na Mohamed Soloka ambao ni wajumbe.
“Bodi inawaalika wanachama wenye mapendekezo zaidi kuhusu marekebisho ya katiba kufika au kuwasilisha katika ofisi za sekretarieti au kupitia barua pepe ya info@simbasc.co.tz kabla ya tarehe 30 Desemba, 2023,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Marekebisho hayo ni miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa pia katika mkutano huo utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC), Dar es Salaam kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Soka Mkutano mkuu Simba Januari 21
Mkutano mkuu Simba Januari 21
Read also