Manchester, England
Kipa wa Man United na timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana anatarajia kukosa mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea ili apate nafasi ya kuichezea Man United katika mechi na Tottenham.
Onana alipewa ruhusa na mabosi wa Shirikisho la Soka Cameroon na kutokuwamo kwenye ziara ya timu hiyo nchini Saudi Arabia ili aweze kucheza mechi ya Man United ya Kombe la FA dhidi ya Wigan iliyochezwa Jumatatu iliyopita.
Baada ya ruhusa hiyo, kipa huyo pia anatarajia kuendelea kuchelewa kwenye timu yake ya taifa ili aweze kuwa golini katika mechi dhidi ya Tottenham itakayopigwa Jumapili ijayo kwenye dimba la Old Traffod.
Katika mechi hiyo, bilionea mpya wa Man United, Sir Jim Ratcliffe kwa mara ya kwanza tangu anunuea hisa asilimia 25 za klabu hiyo, atakuwa jukwaani Old Traffod akiishuhudia timu yake.
Baada ya mechi hiyo ya Old Trafford ndipo Onana atakapoungana na timu ya Cameroon na habari za ndani zinadai kuwa mabosi wa soka Cameroon wamempa ruhusa kuchelewa na hivyo atakuwa kikosini saa kadhaa baada ya mechi ya kwanza ya Afcon dhidi ya Guinea itakayochezwa Januari 15.
Kwa mantiki hiyo, Onana ataanza kuiwakilisha Cameroon kwenye Afcon katika mechi mbili za hatua ya makundi dhidi ya Senegal itakayopigwa Januari 19, na dhidi ya Gambia, Januari 23.
Baada ya hapo uwapo wa Onana kwenye Afcon utategemea kama Cameroon itasonga mbele kwenye michuano hiyo.
Kimataifa Onana kukosa mechi ya kwanza Afcon
Onana kukosa mechi ya kwanza Afcon
Read also