Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouf Dabo amewataka washambuliaji wake kufunga mabao ya kutosha kwani yatawasaidia mbele ya safari kwenye Ligi Kuu NBC.
Davo raia wa Senegal alisema mpaka sasa timu yake ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kutokana na wingi wa mabao waliyofunga jambo ambalo wanapaswa kuendelea kulitilia mkazo.
“Tupo kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya wapinzani wetu Yanga tunaolingana nao kwa pointi kutokana na sare dhidi ya Kagera Sugar jana, nimewaambia washambuliaji waongeze umakini na kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza katika kila mchezo,” alisema Dabo.
Alisema katika ligi yenye ushindani kama hiyo bingwa kupatikana kwa wingi wa mabao si ajabu ndio maana amekuwa akipambana na safu yake ya ushambuliaji kwa kuwa ndiyo iliyoshikilia hatima ya malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Katika michezo 13 iliyocheza ya mzunguko wa kwanza, Azam imefunga mabao 35 na kuruhusu mabao 10 wakati wapinzani wao Yanga waliopo nafasi ya pili wakilingana kwa idadi ya pointi, wamefunga mabao 31 na kuruhusu mabao sita.
Soka Dabo ataka mabao mengi Azam
Dabo ataka mabao mengi Azam
Read also