Manchester, England
Man United inajiandaa kuchukua uamuzi wa kuachana na winga wake Jadon Sancho (pichani) mapema Januari mwakani baada ya mchezaji huyo kutokuwa tayari kumuomba radhi kocha wake, Erik ten Hag.
Sancho hadi sasa hajamuomba radhi Ten Hag baada ya kudai kwamba kocha huyo hakusema ukweli kuhusu sababu za kumuweka benchi katika mechi iliyopigwa Septemba 3 dhidi ya Arsenal na Man United kulala kwa mabao 3-1.
Baada ya Sancho kutoa kauli hiyo, Ten Hag alimtaka mchezaji huyo kumuomba radhi na kutoa taarifa kwa uma lakini hadi sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hajafanya anachotaka kocha wake.
Ten Hag alisema kwamba aliamua kumuacha mchezaji huyo kwa sababu hakuwa katika kiwango bora jambo ambalo Sancho alilipinga akitumia mitandao ya kijamii kudai kwamba kocha huyo ni muongo na alichofanya ni kumtoa kafara.
Na ingawa zipo habari kwamba Ten Hag bado hajamtoa Sancho moja kwa moja katika hesabu zake, kitendo cha mchezaji huyo kukataa kuomba radhi kinaonekana kumchosha na hiyo inaweza kuwa sababu ya kuchukua uamuzi mgumu.
Sancho ametengwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo na hadi sasa anafanya mazoezi ya peke yake huku akikosa ukaribu na wachezaji wenzake wa kikosi hicho na haitoshangaza wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari akapigwa bei.
Sancho alijiunga na Man United mwaka 2021 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya Pauni 73 milioni na ana mkatab unaofikia mwisho mwaka 2026.
Kimataifa Sancho ahesabu siku Man United
Sancho ahesabu siku Man United
Read also
