London, England
Chama cha Soka England, (FA) kinadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Chelsea na Bayen Munich, Thomas Tuchel ili akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya England.
Iwapo mpango huo utafanikiwa Tuchel atakuwa kocha wa tatu wa kigeni kuinoa timu hiyo baada ya Sven Goran Eriksson wa Sweden na Fabio Capelo wa Italia kuwahi kuinoa timu hiyo.
Kwa sasa timu ya England inanolewa na kocha wa muda, Lee Carsley ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu kujiuzulu kwa Gareth Southgate ambaye alidumu kwa miaka minane.
Southgate aliamua kujiuzulu baada ya tmu hiyo kufikia hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Ulaya au Euro 2024 nchini Ujerumani lakini ikashindwa kutamba mbele ya Hispania waliobeba taji.
Taarifa kuhusu mpango huo ilieleza kuwa mazungumzo ya awali na kocha huyo Mjerumani yameshafanyika huku kocha huyo akipewa nafasi kubwa ya kuchukua kibarua hicho.
Tuchel alilazimika kuachana na klabu ya Bayern Mei mwaka huu licha ya kuwa na mwaka mmoja katika mkataba wake lakini aliondoka kwa kuwa mwenendo wa timu haukuwafurahisha mabosi wake.
Kocha huyo ambaye aliiwezesha Chelsea kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mambo yake hayakuwa mazuri Bayern baada ya timu hiyo kushindwa kubeba taji la Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2011-12.
Kimataifa Tuchel kuinoa England?
Tuchel kuinoa England?
Read also
